Joe Cocker
John Robert 'Joe' Cocker (20 Mei 1944 – 22 Desemba 2014) alikuwa mwimbaji wa Uingereza anayejulikana kwa sauti yake ya kwaruzo na yenye hisia za miondoko ya blues (gritty, bluesy voice), pamoja na utumbuizaji wake wa jukwaani wenye nguvu ulioshirikisha miondoko ya mwili yenye kuelezea hisia. Nyimbo zake nyingi zilizovuma zaidi zilikuwa ni marudio (interpretations) ya nyimbo zilizoandikwa na watu wengine, kama vile 'Feelin' Alright' na 'Unchain My Heart', ingawa Cocker alitunga pia nyimbo zake binafsi kwa ajili ya albamu zake nyingi, mara nyingi akishirikiana na mshirika wake wa uandishi wa nyimbo Chris Stainton.[1][2]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Cocker alizaliwa tarehe 20 Mei 1944 katika Barabara ya 38 Tasker, Crookes, Sheffield. Alikuwa mtoto wa mwisho wa kiume wa mtumishi wa umma, Harold Norman Cocker (1907–2001), ambaye wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wake alikuwa akitumikia kama mwanajeshi wa anga (aircraftman) katika Jeshi la Anga la Kifalme (Royal Air Force), na Madge (née Lee). Kulingana na hadithi tofauti za familia, Cocker alipata jina lake la utani la 'Joe' ama kutokana na kucheza mchezo wa utotoni ulioitwa 'Cowboy Joe', au kutoka kwa msafisha madirisha wa eneo hilo aliyeitwa Joe.[3][4][5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1961,[6] chini ya jina la jukwaani la 'Vance Arnold', Cocker alianzisha kikundi kipya kilichoitwa Vance Arnold and the Avengers. Jina hilo lilikuwa mchanganyiko wa Vince Everett (mhusika wa Elvis Presley katika filamu ya Jailhouse Rock, jina ambalo Cocker alilisikia vibaya kama Vance) na mwimbaji wa muziki wa country Eddy Arnold.[7][8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.independent.co.uk/news/people/news/joe-cocker-formidable-vocalist-who-triumphed-at-woodstock-and-won-a-grammy-with-up-where-we-belong-9943221.html
- ↑ http://news.bbc.co.uk/2/hi/entertainment/6758183.stm
- ↑ https://www.oxforddnb.com/display/10.1093/odnb/9780198614128.001.0001/odnb-9780198614128-e-108196
- ↑ https://www.theguardian.com/music/2007/jun/10/popandrock.meltdownfestival2007
- ↑ https://www.theguardian.com/music/2009/apr/19/jarvis-cocker-soundtrack-of-my-life
- ↑ https://web.archive.org/web/20080730171247/http://www.cocker.com/Story1.html
- ↑ https://books.google.co.tz/books?id=Rj5pYWRzoe8C&pg=PA33&redir_esc=y#v=onepage&q&f=false
- ↑ https://www.theguardian.com/music/2014/dec/22/joe-cocker-dies-grammy-winning-sheffield-singer
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joe Cocker kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |